} });
 


Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amesema serikali inaendelea kuwachukulia hatua wala rushwa pamoja na viongozi wanaotumia vibaya fedha za umma kujinifaisha na kukwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa maendeleo ya taifa.

Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Mwanamageuzi kinachozungumzia kipindi cha kwanza cha utawala wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambapo pamoja na mambo mengine amezungumzia mapambano dhidi ya rushwa.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kitabu hicho kitakuwa ni chachu ya historia ya nchi.

Awali akitoa muhtasari wa kitabu hicho, Mhariri Mkuu wa Kitabu, Profesa Ted Maliyamkono amesema miongoni mwa maswala yaliyoandikwa ni pamoja na mapambano dhidi ya rushwa ambayo Dkt. Magufuli amepambana nayo. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top