} });
 


Mazoezi ya kuapishwa (rehearsal) kwa Rais wa Marekani, Joe Biden na makamu wake, Harris Kamala yameahirishwa leo (jana) Jumatatu, Januari 18, 2020 baada ya kutokea tishio la shambulio karibu na eneo ambalo zoezi hilo lilikuwa likifanyika.

Waratibu za zoezi hilo pamoja na vikosi vya usalama wamelazimika kukimbia kutoka katika eneo hilo ambalo limepangwa kufanyika uapisho huo keshokutwa Jumatano, Januari 20, 2021, baada ya kuanza kutokea viashiria vya mlipuko.

Aidha, wamewaelekeza watu wote waliokuwa eneo hilo kuondoka na kukaa mbali na maeneo ya madirishani. Taharuki hiyo imekuja ikiwa ni wiki mbili tangu jengo la bunge la nchi hiyo kuvamiwa na wafuasi wa Rais anayemaliza muda wake, Donald Trump na kufanya vurugu zilizosababisha vifo vya watu wanne na wengine kujeruhiwa vibaya.

Kikosi cha zimamoto na uokoaji kimewahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kuuzima moshi huo uliokuwa ukivuka kutokea kwenye kifusi, chini ya daraja karibu kabisa na eneo la uapisho. Aidha, bado haijafahamika wahusika wa tukio hilo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top