} });
 

 

Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imeteketeza tani 52 za mchele ulioingizwa nchini na Mfanyabiashara Suleiman Abdalla mwezi Machi mwaka jana ukiwa umeshaharibika na haufai kwa matumizi ya binadamu.

Mchele huo ambao ulikuwa umo kwenye makontena mawili bandarini Malindi, ulitakiwa urejeshwe ulikonunuliwa ama uangamizwe kwa gharama za mfanyabiashara mwenyewe na alikubali kugharamia zoezi la kuuangamiza.

Mkurugenzi Idara za Huduma za Maabara wa Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar Nadir Khatib Hassan, ambae alisimamia uangamizaji huo katika jaa la Kibele, alisema uliingizwa nchini tarehe 15.3.2019 kutoka Pakistan.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top