} });
 


Mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa Ruvuma  imevuka lengo la kukusanya kodi kwa kipindi cha julai hadi disemba 2020  kwa kukusanya mapato kwa asilimia 109 na kupewa tuzo ya mkusanyaji bora wa mapato nchini.

Kaimu meneja wa  TRA mkoa wa Ruvuma Bi. Amina Ndumbogani amesema tuzo hiyo imekuwa chachu ya kuongeza bidii kwenye ukusanyaji wa kodi na kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande wake Asa huduma na elimu kwa mlipa kodi  wa mkoa wa Ruvuma Bw. Justine Katiti amesema baada ya kuwapa elimu wafanyabiashara katika mkoa huo wameelewa kuhusiana na kutumia mashine za kielekroniki kutolea risiti (EFD) na pia kulipa kodi bila shuruti. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top