} });
 


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw.Albert Chalamila ameunda kamati huru ili kuchunguza kifo cha dereva wa lori, Abdulrahaman Issa ambaye video yake imeonekana kwenye mitandao ya kijamii akifanyiwa vitendo vya ukatili na askari polisi, tukio ambalo linadaiwa kutokea Mkoani Mbeya.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amesema ameiona video ya dereva huyo kwenye mitandao ya kijamii na ndipo akaamua kuchukua hatua.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amezuia mwili wa marehemu kuzikwa mpaka hapo kamati aliyoiunda ambayo ameipa siku tatu kufanya kazi hiyo itakapokuwa imekamilisha kazi na kutoa taarifa yake.

Mwenyekiti wa Chama cha Madereva, Bw.Hussein Msangi amesema baada ya kuka katika Hospitali ya Igawilo, wamejiridhisha kuwa dereva mwenzao hakua hospitalini, hivyo wakaomba uchunguzi zaidi kuhusu kifo hicho ufanyike. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top