} });
 


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia Televisheni ya Wasafi TV kutoa huduma kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari 6, 2021, hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.

 

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomwonesha msanii wa Bongo, Fleva, Gift Stanford, maarufu kama Gigy Money akicheza utupu kinyume na kanuni za maadili katika tamasha la Tumewasha Live Concert lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

 

Aidha Wasafi TV wanatakiwa kutumia siku ya leo kuomba radhi kwa watazamaji wake kufuatia ukiukaji huo na wakikaidi hatua zaidi za kisheria na udhibiti zitachukuliwa.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top