} });
 

 

Jeshi la polisi Mkoani Arusha limewaua kwa kuwapiga risasi watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi waliokuwa wakitafutwa kwa muda mrefu kuhusiana na matukio ya uhalifu wa kutumia silaha.

Tukio hilo limetokea Januari 07, 2020 mchana katika mtaa wa Manyara kata ya Sombetini baada ya majambazi hao kukutwa wamejificha katika nyumba moja ya inayouzwa pombe za kienyeji.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha ,Salumu Hamduni amethibitisha tukio hilo na kusema kuwa atatoa taarifa zaidi hapo baadaye baada ya kupata taarifa kamili kutoka kwa wasaidizi wake

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top