} });
 

 

PENGINE  haikuchukua muda mrefu kwa Tiziana Cantone kuanza mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kujikatisha uhai.

 

Mwezi Aprili mwaka 2015, mwanadada kutoka Mugnano, nje kidogo mwa Naples, alituma picha za video za ngono kupitia WhatsApp. Waliopokea video hizo miongoni mwao ni rafiki yake wa kiume, Sergio Di Palo, ambaye mahusiano yake naye hayakuwa mazuri.

 

Video hizo zilimuonyesha Tiziana akifanya vitendo vya ngono na wanaume kadhaa ambao hawakufahamika. ‘

 

‘Alikuwa mrembo lakini mwenye kuvunjika moyo upesi,”alikumbuka Teresa Petrosino ambaye walikuwa marafiki kwa miaka 15.” Alikuwa na watu wasiofaa kwa wakati usiofaa.”

 

Video hizo zilisambazwa kwenye tovuti mbalimbali zinazoonyesha masuala ya ngono. Vitendo vyenyewe kwenye video hizo havikuwa kitu isipokuwa sentensi moja tu kutoka mdomoni mwa Tiziana Conte. ”Unarekodi video?” alimuuliza mwanamme aliyekuwa ameshika Kamera.

 

Maneno hayo yaliashiria kuwa mwanadada huyo anapenda kupigwa picha wakati akifanya ngono. Sentensi hiyo ilifanya watazamaji waendelee kuitazama bila wasiwasi. Kama alikua anafurahia kupigwa picha, bila shaka hatachukia watu wakiitazama.

 

Lakini Waitaliano walifanya zaidi ya kutazama.      Watazamaji walitumia maneno yake kwa msisitizo wakatengeneza t-shirt ambazo ziliwekwa picha yake na pia kwenye tovuti. Hakuna aliyekuwa akifikiria kuwa Tiziana asingependa, kwa kuwa alionekana kufurahia kwenye video hizo.

 

Lakini mambo hayakuwa hivyo

”Watu huchanganya kukubali jambo, na jambo hilo kusambaa zaidi,” anaeleza mtaalamu wa masuala ya mitandao, Selvaggia Lucarelli.


”Unaweza kupiga picha ya video, ukawaonesha watu kadhaa, lakini kunakuwa na makubaliano kuwa watu hao wasisambaze zaidi.”Mapambano ya kisheria

Tiziana Cantone, aligopeshwa sana na hali hii. ”Mimi na yeye hatukuwahi kuongea kuhusu kilichomo kwenye video,” alisema rafiki yake Teresa.”Sikuwahi kuziona, na sikutaka kuziona.    Unaweza kuona alikuwa akisumbuka mno.   Lakini alikuwa na nguvu.”

 

Bi Cantone akaamua kupambana.Lakini hakukua na njia ya haraka ya kufanya ili kuondosha video hizo. Aliipeleka kesi mahakamani, akidai kuwa video hizo zilipelekwa kwenye mitandao bila ridhaa yake.Lakini mpaka wakati huo hakuweza kuishi maisha ya kawaida.

 

”Hakutaka kutoka nje akiogopa watamuona.” Alieleza Teresa. ”Alielewa kwa kiasi fulani kuwa hali hii haiwezi kutatulika;kuwa mume wake,watoto wake wanaweza kuziona video hizo siku moja;na kuwa video hizo hazitaondoka mitandaoni.”

 

Ilimchukua wiki kadhaa Mama yake Teresa Giglio kupata nguvu kuwaambia wanahabari kuhusu maisha ya binti yake. ”Binti yangu alikuwa na tabia njema lakini pia alikuwa na mapungufu yake,” aliiambia BBC. ”Hakuwa na mapenzi ya baba, tangu alipozaliwa.   Hakuwahi kumuona baba yake.    Hii iliathiri maisha yake.”

 

Mama na mwana waliishi pamoja.    Katika kipindi cha furaha, Tiziana alipenda kusikiliza wanamuziki wa Italia, kusoma vitabu vya simulizi, kupiga kinanda.    Lakini baada ya video kutapakaa mitandaoni hali hiyo haikuwepo tena.


”Maisha yake yaliharibika, mbele ya kila mtu,” alisema mama yake.       ”Watu walimfanya kichekesho ,akaitwa majina mabaya ya aibu.”

 

Mwezi Septemba, Mahakama ya Naples iliamuru video hizo zitolewe mitandaoni na kwenye tovuti.Lakini ilimtaka Tizianz alipe faini ya dola 21,600 za Marekani, gharama za huduma za kisheria.     Fedha ilikuwa nyingi sana. Tarehe 13 mwezi Septemba mwaka 2016, Maria Teresa Giglio alikwenda kazini, akiwa amemuacha binti yake nyumbani.

 

Bi Giglio alipokea simu kutoka kwa wifi yake ,   sauti ikiwa ya kupoa sana ikimtaka arejee nyumbani. Aliporejea alikuta polisi, gari la kubeba wagonjwa, ”haraka nikaelewa’ ‘alisema , huku akilia. ”Siku alipokufa maisha yangu yalikomea hapo.”Nani aliweka video Mtandaoni?

Kitendo cha Tiziana Cantone kujitoa uhai, kilifanya video hizo zifuatiliwe na watu wengi zaidi kuliko kusahaulika. Mama yake alijilazimisha azitazame video hizo.

 

”Nilitaka kuona kila kitu ili niweze kuuelewa ukweli.” huyu hakua Tiziana wangu” alishawishika kuwa binti yake alikua anatumia dawa za kulevya.

 

Bi Giglio amemtaka mpenzi wa zamani wa binti yake, Di Pialo, kueleza hasa alishiriki vipi katika mpango wa kusambaza video zile. ”Hakunisaidia kuokoa maisha yake.Lakini labda anaweza kunisaidia kupata ukweli.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top