} });
 


Shirikisho la wafanyabiashara wa India (CAIT) limeiomba Serikali izuie mtandao wa WhatsAppFacebook na Facebook Messenger kutokana na sera mpya ya Faragha.

 

Wamemuandikia Waziri wa Habari na Teknolojia kuwa India ina watumiaji zaidi ya milioni 200 hivyo kuchukua taarifa zao kwa matumizi ni hatari kwa uchumi wa nchi.

 

Aidha, wamesema kuchukua taarifa za manunuzi na taarifa nyingine sio mbaya tu kwa Uchumi bali pia hata usalama wa nchi unaweza kuwa mashakani.

 

CAIT wamesema sera mpya ya faragha ya WhatsApp inakiuka misingi ya faragha na ipo kinyume na masuala ya msingi yaliyo kwenye Katiba ya India.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top