} });
 

 

WANANCHI wa mtaa wa Mwananchi kata ya Mahina Wilayani Nyamagana mkoani Mwanza, wameifunga ofisi ya mtaa huo, wakishinikiza Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kuwaweke viongozi wengine katika kiti cha uwenyekiti kufuatia chama hicho kumsimisha uanachama Mwenyekiti wa mtaa wao.

 

Wàkizungumza na waandishi wa habari wananchi wa mtaa huo ambao waliandamana hadi ofisini ya mtaa, kwa lengo la kuutaka uongozi wa juu kuingilia kati, suala la wajumbe waliosimamiswa amabo ni Emanuel Lubuya, John Maritin, Juma Sumuni na Dorothi Sekito ambao walitaka kujitwalia madaraka bila utaratibu wowote kwa kigezo cha kurudishwa madarani na CCM.

 

“Tunashangaa kuona wajumbe wa mtaa wanne ambao walivuliwa madaraka na mkutano mkuu wa mtaa, kufuatia ubadhirifu wa fedha za mfuko wa mahafa na wizi wa mifuko ya Saruji, wanafika ofisi ya mtaa wanaanzisha vurugu,wakimtaka mwenyekiti Catherine Thomas, awakabizi mhuri na nyaraka za ofisi kwa madai kuwa hana sifa ya kuwa Mwenyekiti kufuatia kusimamishwa uanachama na Chama chake,” alisema Daniel Said kwa niaba ya wananchi wenzake.

 

Aidha, wananchi hao walisema wanashangaa kwanini Viongozi wa CCM wanavutana na mwenyekiti wa mtaa ambaye wao ndio waliyemteua katika vikao vyao vya Chama, maana walikata majina ya walioshinda waka mrudisha yeye.

 

“Tunauomba uongozi wa CCM wa juu pamoja na serikali waingilie kati wafanye uwamuzi wa suala hili,maana hapa kunauonevu unaofanywa juu ya mwenyekiti tunashindwa kuelewa kosa lake ni kufanya maendeleo walitaka fedha zinazopatikana kutoka kwa wadau wazigawane maana hii vurugu hatuelewi inatokana na nini maamuzi ni ya wananchi tena kwenye mkutano halali sasa kosa la Catherine nini,” alisema Salimu Athumani.

 

Wananchi hao wamedai kuwa mwenyekiti huyo wa mtaa ni mchapakazi maana ni muda mchache wa mwaka mmoja tangu ajaguliwe amefanya maaendeleo tofauti na viongozi wa mtaa waliopita.

 

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwananchi, Catherine Thomas alisema uongozi wake umekuwa na changamoto kutokana na msimamo wake wa kugoma kugawia fedha baadhi ya viongozi wa CCM ngazi ya kata, zinazopatikana kutoka kwa wananchi na wadau.


“Kinachoniponza mimi ni kutokukubaliana na maelekezo ya viongozi wangu wa Kata ya Mahina wa CCM, kutokana na kukataa kutoa fungu la fedha ambazo tunakusanya kutoka kwa wadau wa viwandani waliopo katika eneo letu, nikafungu akaunti ya Serikali ya mtaa na kuweka fedha zote huko, zikitakiwa kwa ajili ya maendeleo zinatoka kwa utaratibu wa mitathari ya vikao halali,” alisema Catherine.

 

Aidha, Catherine alisema kutokana na msimamo wake,ulipelekea kuwepo na mgawanyiko baina yake na wajumbe, wanne walifuata maelekezo ya kiongozi wa CCM kata na mmoja alibaki akimuunga mkono, hivyo kutokana na hali hiyo aliitwa na uongozi wa CCM wa kata yake katika kikao ambacho kilitoa maamuzi ya kumvua uanachana ili kupoteza sifa ya kuwa Mwenyekiti kwa manufaa yao.

 

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Godfray Kavenga alisema kufuatia sakata la mwenyekiti kukiuka kanuni za Chama kwa kuwapeleka wajumbe wake kwa wananchi wakavuliwa madaraka, hivyo walielekeza Mwenyekiti Catherine asimamishwe uanachama ili taratibu zifuuatwe.

 

“Mwenyekiti wa mtaa wa Mwananchi Catherine alikizalilisha Chama kwa kuwashitaki wajumbe wake wanaotokana na CCM kwa wananchi hadi wakavuliwa madalaka, wakati alitakiwa kupeleka malamiko yake katika uongozi wa CCM tawi lakini hakufanya hivyo, kutokana na utovu wa nidhamu ndani ya Chama atasimama kwa mwanachama na kuhudumia wananchi hadi vikao viitakapo kaa,” alisema Kavenga.

 

Akizungumzia kuhusu kusimamishwa kwa mwenyekiti huyo wa mtaa mkurugenzi wa Jiji Kiomoni Kibamba alisema yeye bado hajapokea barua yoyote ya kumsimamisha au kumvua uanachama Carherine kutoka CCM hivyo hawezi kuzungumza chochote.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top