} });
 


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mhe. Selemani Jafo, ameipongeza Halmashauri ya Buchosa, Sengerema mkoani Mwanza kwa kutekeleza miradi ya ujenzi wa jengo jipya la halmashauri hiyo lenye ghorofa moja  na Kituo cha Afya cha Isaka.

Amesema hayo leo Jumanne, Januari 05, 2021,  alipofanya ziara na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika halmashauri hiyo.

Amesema ujenzi wa halmashauri pamoja na zahanati inayotekelezwa nchi nzima, Buchosa inaongoza kwa kujenga majengo yenye viwango vinavyoendana na thamani ya fedha zilizotolewa na serikali.

Aidha, katika ziara hiyo, Jafo amezungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kuwataka wafanye kazi kwa ushirikiano na kuacha tabia ya kugombana kati ya idara na idara nyingine ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi zao.

Pia, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kuwezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa haraka pamoja na kurahisisha utendaji kazi kwa watumishi na uendeshaji wa halmashauri hiyo.

Katika ziara yake, Jafo aliongozana na timu yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, na kupokelewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  na Mbunge wa Buchosa, Mhe. Eric Shigongo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top