} });
 


Waziri Mkuu wa Mongolia Khurelsukh Ukhnaa amewasilisha barua ya kujiuzulu mbele ya Bunge leo kufuatia maandamano ya umma kulaani jinsi Serikali yake inavyoshughulikia janga la virusi vya Corona.

Shirika la Habari la Taifa limeripoti kuwa Ukhnaa amesema anachukua uamuzi huo kama sehemu ya kuwajibika na kuitikia matakwa ya umma yaliyochochewa na kile kinachotajwa kuwa unyanyasaji kwa wagonjwa wa COVID-19.

Maandamano makubwa yalizuka Jumatano Januari 20, 2021  baada ya kuvuja kwa mkanda wa video ulioonesha mwanamke mmoja na mtoto wake mchanga wakihamishwa kwa nguvu kwenda kituo cha karantini kinachoendeshwa na idara ya afya ya taifa.

Maandamano hayo yamechochea pia kujiuzulu kwa viongozi wengine wa serikali ikiwemo waziri wa afya na naibu waziri mkuu kwenye taifa hilo lenye zaidi ya visa 1,500 vya COVID-19.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top