} });
 


IKIWa ni siku moja tu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kutaka Wizara ya Afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka Tanzania kujiandaa kupokea na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.

 

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na Kanda ya Afrika mashariki kwa ujumla.

 

”Tumeanza kuwasiliana upya na ngazi za juu za uongozi, na tunatoa mchango wetu kama ilivyokua hapo mwanzo, na tunataka kushirikiana na Tanzania, kwa niaba ya watu wa Tanzania, nchi jirani na dunia kwa ujumla. Sehemu ya mawasiliano yetu na Tanzania ni kukumbusha serikali kuwa, hii ni sehemu ya makubaliano ya kanuni za afya za Kimataifa ambapo nchi wanachama wamekubali kwa pamoja kuzuia kusambaa kwa magonjwa,” anasema Dkt. Moeti.

 

 

WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona. Shirika hilo pia limesisita Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.

 

”Moja ya makubaliano ya wanachama ni kutoa takwimu za mwenendo wa ugonjwa, nimewakumbusha serikali ya Tanzania na ninayo kumbukumbu kwa maandishi kuwa wao ni sehemu ya wanachama hivyo wanatakiwa kuitikia wito huu. Tuna imani kuwa mawasiliano yetu kuhusu chanjo yatazingatiwa ili kukabili maambukizi ya virusi,” ameongezea Dkt. Moeti.

 

Naye Katibu Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Tedros Ghebreyesus anasema anaunga mkono alichosema @MoetiTshidi, anatoa rai hatua dhabiti za kiafya kukabiliana dhidi ya corona zinapaswa kufuatwa na kujiandaa kupokea chanjo.

 

Takwimu ni suala la muhimu pia kwa Tanzania kuzitoa , tena baada ya kesi za miongoni mwa wasafiri na wageni katika miezi ya hivi karibuni. Hatua hii ya WHO inakuja siku moja baada ya Rais wa Tanzania John Magufuli kutahadharisha kuhusu chanjo ya Covid 19 ambayo imeanza kutolewa katika mataifa mbalimbali duniani.

 

Alipozungumza katika uzinduzi wa shamba la miti huko wilayani Chato mkoani Geita, alizungumzia pia kuhusu hali ya corona nchini na kuwasihi wananchi kuendela kuomba pamoja na kujifukiza. ”Tutaendelea kuchukua tahadhari, pamoja na kujifukiza, kusali na kuswali, huku tukiendelea na shughuli zetu, ule vizuri ushibe corona ashindwe kuingia kwenye mwili wako”.

 

Aidha kuhusu uwepo wa aina mpya ya corona Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya Watanzania walienda kupata chanjo huko nje lakini wakaletea aina mpya ya corona. ”Ninajua Kuna baadhi ya Watanzania hata wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na walivyochanjwa wakaja huku wakatuletea corona ya ajabu ajabu”. Alisema Rais Magufuli.

 

Rais Magufuli alisisitiza juu ya madhara ya chanjo, hususani kuwa hakuna chajo za magonjwa sugu ya muda mrefu kama UKIMWI na saratani. ”Tusiwe tunakimbilia masuala chanjo chanjo, si kila chanjo ina faida kwetu, ni lazima Watanzania tuwe macho, tuwe waangalifu, tutafanyiwa majaribio, tuendelee kumuomba Mungu wetu na tuendelee kuchukua tahadhari”.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top