} });
 

 

KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amesema uwepo wa beki mkongwe, Kelvin Yondani kwenye kikosi chake, umeongeza umakini kwenye safu yake ya ulinzi.

 

Juzi Jumanne, Polisi Tanzania ilifanikiwa kutinga hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC, huku Yondani akicheza mchezo wake wa kwanza kikosini hapo tangu asajiliwe kipindi hiki cha dirisha dogo.


Malale amesema: “Kuwa na mchezaji mzoefu kama Yondani kwenye kikosi ni jambo zuri kwani ni mchezaji ambaye amecheza kwa kiwango cha juu kwenye timu kubwa, hivyo uzoefu wake utakuwa msaada mkubwa kwetu kutokana na kikosi chetu kuwa na idadi kubwa ya vijana.“

Tulikuwa na tatizo kwenye safu yetu ya ulinzi jambo ambalo lilipelekea tuwe tunaruhusu mabao mepesi kwenye mechi zetu, hivyo uwepo wa Yondani kikosini kwa kiasi kikubwa utaongeza umakini kweye safu ya ulinzi kutokana na uzoefu alionao.”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top