} });
 


Halmashauri ya wilaya ya Geita imeanza kugawa mifuko zaidi ya mia moja ya saruji katika kila kata ili kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyoanzishwa na wananchi vinakamilika kwa wakati kuwawezesha wanafunzi kusoma.

Akizungumza na wadau wa elimu katika eneo la Nzela, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Donald Nnsoko amesema mpango huo utasaidia kupunguza uhaba wa vyumba vya madarasa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita Charles Kazungu amesema upungufu wa vyumba vya madarasa katika halmashauri hiyo umetokana na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaotokana na elimu bure. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top