} });
 


RAPA nguli nchini Marekani, Curtis James Jackson maarufu kama ’50 Cent’ amesema anataka kuingia ulingoni kuzichapa na bondia bingwa wa Dunia, Floyd Mayweather.

 

Kwenye mahojiano yake kupitia V-103 “The Morning Culture”, 50 Cent aliulizwa ni nani anataka kupigana naye kwenye pambano la masumbwi na hakusita kumtaja hasimu wake huyo wa muda mrefu.


“Nitapigana na Floyd. Lakini hofu yangu ipo kwenye uzito, sijui kama naweza kufanana naye,” alisema rapa huyo na mfanyabiashara.

 

50 Cent aliwahi kuwa memba wa karibu na Mayweather na hata kuingia naye ulingoni siku ya pambano na Oscar De La Hoya. Wawili hao walikuja kupishana kutokana na kutokubaliana kibiashara.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top