} });
 

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limefungua jalada la uchunguzi kwa Hospitali ya Aga Khan ya jijini humo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wanatozwa gharama kubwa za matibabu kwa wagonjwa wa matatizo ya ‘Pneumonia’ yanayopelekea matatizo ya upumuaji.

Taarifa hiyo imetolewa Februari 18, 2021, na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo SACP Lazaro Mambosasa, na kuongeza kuwa pia wanaopatiwa matibabu katika hospitali hiyo pindi wanapofariki kumekuwa na tabia ya kuzuia miili ya marehemu na kudai kiasi kikubwa cha fedha kinyume na maelekezo ya serikali.

Aidha SACP Mambosasa, ameongeza kuwa uchunguzi huo utakapokamilika na kubaini tuhuma hizi ni za kweli hatua kali za kisheria zitachukuliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto dhidi ya Hospitali hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top