
Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Fredius Philibart Kibengo mkazi wa Omurushaka
wilayani Karagwe kwa tuhuma za kumuua mama yeke mzazi kwa kumkata shingoni kwa
kutumia kitu chenye ncha kali baada ya mganga wa kienyeji kumtaka kupeleka damu ya mama yake au ndugu yake wa karibu ili kutengenezewa dawa za kuongeza utajiri kwenye
biashara.
Katika uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi mkoani Kagera umebaini kuwa katika kipindi cha
siku chache kabla ya tukio hilo kutokea mtuhumiwa alisari kuelekea nchini Burundi kutafuta
dawa za kuongeza utajiri na aliporejea nyumbani kwake alimshirikisha mkewe kuhusu
mashariti aliyopewa na waganga wa kienyeji lakini mke wake hakukubaliana na masharti hayo.
Hata hivyo Februari 17 mwaka huu mtuhumiwa alionekana maeneo ya nyumbani kwa mama
yake mzazi na ilipoka usiku wa kuamkia Februari 18 alimvamia mama yake na kumkata na
kitu chenye ncha kali kisha kupoteza maisha.
Hata hivyo kamanda malimi amewataka wakazi wa mkoa wa kagera kujiepusha na imani za
kishirikina ambazo zimekuwa zikichangia mauwaji ya wananchi wasio na hatia.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment