} });
 


Wakili H├ęctor Cipriano Paredes amezua gumzo nchini Peru na duniani kwa ujumla mara baada ya kufanya ngono na mwanamke mmoja wakati kesi ikiendelea kusikilizwa kwa njia ya video mtandaoni.

  

Paredes alianza kuvua nguo kisha kufuatiwa na mwanamke aliyekua nae na kuanza kufanya tendo hilo wakati mkutano huo ukiendelea mubashara. Video ya tukio hilo imesambaa kwenye mtandao wa Twitter.

  

Tukio hilo lilikua likishuhudiwa moja kwa moja na majaji, mawakili na baadhi ya wafuatiliaji wa kesi hiyo. Paredes alikua wakili wa upande wa mshitakiwa katika kesi iliyohusisha kundi la wahalifu linaloogopewa nchini humo. 

 

Jaji John Chachua Torres aliyekua akiendesha kesi hiyo, alisitisha mara moja kusikilizwa kwa kesi hiyo na kusema kuwa wakili Paredes ameikosea heshima mahakama.

 

Baada ya Jaji Torres kujiridhisha kuwa ilikua ni camera ya Paredes, aliamuru mara moja wakili huyu aanze kuchunguzwa na asimamishwe kushiriki katika kesi hiyo. 

 

‘’Tunashuhudia kitendo cha udhalilishaji na kinaoneshwa moja kwa moja hapa, hivyo kitengo cha uchunguzi nataka wakili huyu achunguzwe mara moja’’ alisema Torres. 

 

Baada ya usikilizwaji wa kesi hiyo kusitishwa. Jaji Torres aliongeza katika taarifa iliyotolewa kwa maandishi kuwa kuanzia sasa wakili Paredes anatambulika kama mtu ambae ametia aibu mahakama, mawakili wenzake na tasnia ya sheria kwa ujumla.

  

Hadi sasa wakili Paredes hajatoa maelezo yoyote baada ya tukio hilo. Mwezi Septemba , mbunge mmoja huko Argentina alijiuzuru mara baada ya kuonekana akibusu matiti ya mwanamke wakati wa kikao cha bunge kilichofanyika kwa njia ya mtandao wa video.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top