} });
 


Safari ya A.Y nchini Marekani imeendelea kutuacha na maswali kichwani, alianza kwa kutuonesha akiwa na waigizaji wakali wa Hollywood, Robert Davi na Richard Grieco na kusema kuwa anafanya filamu na wakongwe hao.

 

Jana aliendelea kutuwekea maswali mazito kichwani kwani alituonesha screenshot akifanya mazungumzo na Baba mzazi wa mwimbaji hodari wa dunia, Rihanna

 

Kupitia Insta stories, A.Y aliweka picha inayomuonesha akifanya mazungumzo ya video na mzee huyo na kuandika “Mazungumzo mazuri na Baba wa Rihanna, Ronald Fenty.” Ni kipi A.Y anapanga kukifanya kupitia mzee huyo? tunasubiri kauli yake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top