} });
 


MTEGO uliowekwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMD) Kanda ya Kusini umefanikiwa kumnasa Jamaly Sad na mtoto wake wakiuza dawa za serikali.

 

Taarifa ya @tmdatanzania inaeleza kwamba Sad amenaswa kwenye mtego huo Januari 31 , 2021 wilayani Newala  akiuza dawa za aerikali za Mpango wa Uzazi.

 

Dawa hizo ni Medroxy Progesterone (vichupa 60) na Microgynon pills (vidonge 3360) zote zikiwa na thamani ya Sh. 300,000.

 

Wawili hao wamefunguliwa jalada polisi RB No. NL/RB/94/221 kuhusu tuhuma hizo na watachukuliwa hatua za kisheria.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top