} });
 


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Korogwe mkoani Tanga nchini Tanzania, Kwame Daftari amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne Februari 16, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini Ofisi ya Rais Tamisemi, Nteghenjwa Hosseah imesema mkurugenzi huyo alifariki dunia jana Jumatatu.

 

“Waziri wa Nchi Tamisemi (Selemani Jafo) anatoa pole kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, wananchi, familia ya marehemu, ndugu na jamaa wote walioguswa na msiba huu,” amesema Nteghenjwa.

 

Taarifa hiyo imesema Daftari aliteuliwa na Rais John Magufuli kushika nafasi ya ukurugenzi katika wilaya hiyo Agosti 13, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo aliwahi kufanya kazi katika sehemu mbalimbali nchini.

 

Nteghenjwa amemkariri Jafo akisema Serikali inatambua na itaendeleza kuenzi mchango wa Daftari katika ujenzi wa Taifa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top