} });
 

 

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, leo (jana) amesema kuwa walioandamana na kulivamia eneo la kihistoria la Red Fort mjini New Delhi wameifedhehesha Nchi hiyo.

Matamshi hayo ya Modi aliyoyatoa kupitia hotuba iliyorushwa moja kwa moja na vituo vya redio ni ya kwanza tangu kuzuka kwa malalamiko ya wakulima ambayo mapema wiki hii yaligeuka kuwa vurugu.

Siku ya Jumanne, ambayo ilikuwa Sikukuu ya Jamhuri Nchini India, maandamano yaliohusisha trekta yaligeuka kuwa ghasia baada ya waandamanaji kukabiliana na Polisi na hatimaye kuvamia eneo hilo la kihistoria.

Mtu mmoja aliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa, Maelfu ya wakulima wamekuwa wakipiga kambi kwenye viunga vya Mjii Mkuu wa Nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili kulalamika kuhusu Sheria za kilimo ambazo wanasema zinawanufaisha wanunuzi binafsi badala ya wazalishaji mazao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top