
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amesema alitamani stendi ya
mabasi ya Mbezi iitwe Magufuli, jina ya Rais wa Tanzania, John Magufuli licha
ya kuwa hakumueleza wazo lake hilo.
Mbunge
huyo wa Kisarawe ameeleza hayo leo Jumatano Februari 24, 2020 mbele ya Rais
Magufuli aliyekuwa akizindua kituo kikuu cha mabasi cha Mbezi ambacho sasa
kinaitwa kituo cha mabasi cha Magufuli.
“Stendi
hii hukuomba mkopo kokote, ni maelekezo yako kati ya Sh360 bilioni
zilizoelekezwa katika miradi mikakati. Kati ya fedha hizo Sh186 bilioni
ulizielekeza katika ujenzi wa stendi 18 za kisasa ndani ya Tanzania, haijawahi
kutokea. Ndio maana mheshimiwa Rais mimi leo nikuombe radhi kwa jambo moja
lakini nafahamu viongozi wa dini wameshapiga dua zao zimekaa vizuri.”
“Ulipokuja
kufungua kile kibao, umekutana na stendi ya mabasi ya Magufuli. Nikasema
haiwezekani hata kidogo uwekezaji mkubwa kama huu ambao watu kutoka nchi
mbalimbali wakija hapa watashangaa. Nilitamani jina lako libaki hapa Dar es
Salaam kwa stendi hii.”
“Ndio maana mheshimiwa Rais nilikuwa naomba Mungu wakati kibao kile kinafunuliwa maana kilifunikwa, nilivyoona kimeandikwa stendi ya mabasi Magufuli nikasema basi Mungu nisitiri sikukuomba,” amesema Jafo.
Post a Comment