} });
 

 

JESHI la Myanmar limetangaza hali ya dharura likidai kufanyika udanganyifu wa kura katika uchaguzi, baada ya kuwakamata viongozi kadhaa akiwemo Aung San Suu Kyi.


Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Myawaddy kinachomilikiwa na jeshi, pia jeshi limetangaza hali ya dharura kwa muda wa mwaka mmoja na kumweka jenerali wa zamani kama rais, na jenerali wa zamani, Myint Swe, ambaye awali alikuwa makamu wa rais, ametangazwa kama kaimu rais.Hata hivyo, katika hali hiyo ya dharura kamanda mkuu wa jeshi, Min Aung Hlaing, amechukua udhibiti kamili wa nchi hiyo. Tangazo hilo la jeshi limetolewa kufuatia kukamatwa kwa kiongozi wa Myanamar, Aung San Suu Kyi, baada ya siku kadhaa za mivutano nchini humo iliyozua hofu ya kutokea mapinduzi.

 

Rais Win Myint na viongozi kadhaa wa ngazi za juu wa chama tawala pia wamekamatwa mapema Jumatatu, amesema Myo Nyun msemaji wa chama hicho cha National League for Democracy.

 

Akizungumza kwa njia ya simu na shirika la habari la DPA, Nyun amesema wakati wowote naye anaweza kukamatwa na wanajeshi hao. Tangu wiki iliyopita jeshi la Myanmar limekuwa likitishia kufanya mapinduzi kwa madai kwamba kulifanyika udanganyifu katika uchaguzi uliopita wa mwezi Novemba uliokipa ushindi chama cha Suu Kyi cha NLD.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top