} });
 

 

Katibu tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega amefariki katika ajali ya gari jana Jumatano Februari 3, 2021 wakati akitoka mkoani humo kwenda Dodoma baada ya gari alilokuwa amepanda kugongana na basi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joseph Mkirikiti amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdori Mizani.

Amesema katika ajali hiyo watu wengine wanne wamejeruhiwa ambao ni dereva wa katibu tawala huyo na wanawake watatu waliokuwa kwenye basi.

“Ni ajali mbaya kumpoteza katibu tawala na muda huu tunajiandaa kurejesha mwili Arusha bado tupo kituo cha afya hapa Magugu,” RC Arusha

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top