} });
 


Waziri wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda na naibu wake, Hussein Bashe wamewasili wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro kusimamia shughuli ya kuwadhibiti nzige walioingia jana wilayani humo.

 

Nzige hao waliingia wilayani humo jana Jumanne Februari 24, 2021 wakidaiwa kutoka wilayani Longido na kuonekana maeneo mbalimbali, tayari ndege kwa ajili ya kuwadhibiti imeanza kufanya kazi. 

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Februari 24, 2021 Profesa Mkenda amesema Serikali imejipanga kutumia nguvu kubwa kuwaangamiza nzige hao.

  

“Hili kundi la nzige walioingia hapa Siha inaonekana wametokea Longido kwa hiyo tulichokifanya asubuhi tumemwaga sumu kuwaangamiza nipo hapa na naibu waziri wangu kuhakikisha tunatumia nguvu kubwa kuwaangamiza.”

 

“Tutahakikisha nzige wote wanaangamia ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kilimo kama kawaida, niwaondoe hofu wananchi wa Siha na Tanzania kwa ujumla hawa nzige baada ya siku mbili wote tutakuwa tumeshawaangamiza,” amesema Profesa Mkenda.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top