
Rais
wa Tanzania, John Magufuli ametaka wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga
kuruhusiwa kufanya biashara katika kituo cha mabasi cha Mbezi.
Kituo
hicho ambacho sasa kinaitwa kituo cha Magufuli kimezinduliwa leo Jumatano
Februari 24, 2021 na kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Amesema
wakati stendi hiyo ikitarajia kupokea mabasi 3,000, abiria watahitaji huduma na
si wote wataingia katika kituo hicho, hivyo wamachinga watakaouza vyakula
wanaruhusiwa wakiwemo mama lishe kwani Serikali ya sasa inajali wananchi.
“Vitu
vilivyomo hapa havitamsaidia mmachinga hataingia mle, sasa nitoe wito kwako
waziri na mkurugenzi mmenipa jina nalikubali kwa ajili ya kuwatetea hawa watu,
nataka niwe balozi wao, nataka itakavyoanza hawa wamachinga wasifukuzwe kwa
sababu ni kwao, mkiandika jina Magufuli stendi halafu wamachinga wakawa
wananyanyaswa hapa sihitaji hilo.”
“Nikueleze Waziri (Selemani Jafo- Tamisemi) inawezekana umejichongea kwa kuiita hii stendi jina la Magufuli, nataka yafanyike haya ambayo Magufuli ninataka yafanyike. Wananchi waruhusiwe mpanue maeneo,” amesema.
Post a Comment