} });
 

 

MAHAKAMA ya talaka ya Beijing imemuamuru mwanaume kumlipa fidia mke wake kwa kazi alizofanya katika kipindi chote walichooana, katika uamuzi wa kihistoria ulioleta mabadiliko katika sheria za nchi hiyo. Mwanamke huyo atapokea Yuan 50,000 sawa na dola 7,700 kwa miaka mitano aliyofanya kazi za nyumbani bila malipo.

 

Kesi hiyo imeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu thamani ya kazi za nyumbani, huku baadhi wakisema kuwa fidia aliyopewa mwanamke huyo ni kiasi kidogo sana. Hukumu hiyo inakuja baada ya Uchina kuanzisha sheria mpya zinazohusu jamii. 

 

Kulingana na rekodi za mahakama , mwanaume aliyetambulishwa kwa jina pekee la ubini kama Chen alikuwa amewasilisha kesi ya talaka dhidi ya mke wake kwa jina la ubini Wang, baada ya kuoana mwaka 2015. 

 

Mwanzoni alisita kumtaliki, lakini baadae aliomba fidia ya pesa, akidai kuwa Chen alikuwa hajafanya kazi yoyote ya nyumbani au kuwajibika vyovyote kwa matunzo ya mtoto wao wa kiume. 

 

Mahakama ya wilaya ya Fangshan mjini Beijing ilimuamrisha kumlipa yuan 2,000 kila mwezi, na malipo ya yuan 50,000 mara moja kwa kazi za nyumbani ambazo alizifanya wakati alipokuwa ameolewa. 

 

Jaji Mkuu katika kesi hiyo aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kuwa mali za pamoja za wawili hao walizopata wakati wa ndoa kwa kawaida hugawanywa sawa baina yao. “Lakini kazi za nyumbani ni mali ilisiyoweza kuhesabika,” alisema jaji. 

 

Hukumu hiyo ilitolewa kulingana na sheria mpya ya makosa ya kiraia, ambayo ilianza kutumika mwaka huu. Chini ya sheria hiyo mpya, mke au mume ana haki ya kudai fidia katika talaka iwapo anafanya majukumu zaidi katika malezi ya mtoto, kumtunza ndugu mzeena kumsaidia mke au mume wake kazi. 

 

Awali , wanandoa waliotalikiana, wangeweza kuomba tu aina hiyo ya fidia kama makubaliano kati yao yangekuwa yamesainiwa na wote wawili- jambo ambalo sio la kawaida kufanyika nchini Uchina. 

 

Katika mitandao ya kijamii, kesi hii imeibua mjadala mkali, huku kampeni katika mtandao wa Weibo iliyotumia alama ya leri ikitazamwa zaidi ya mara milioni 570. 

 

Watumiaji wa mitandao ya kijamii walisema kuwa yuan 50,000 kwa miaka mitano ya kazi ni pesa kidogo sana . “Sina la kusema, kazi ya wakati wote ya mke wa nyumbani inapuuzwa. Mjini Beijing, kumuajili mfanyakazi wa nyumbani kwa mwaka inagarimu yuan 50,000 ,” alisema mchangiaji mmoja wa maoni kwenye mtandao wa kijamii. 

 

Wengine walisema kuwa wanaume wanapaswa kuwajibika kwa majukumu zaidi ya nyumbani. Baadhi pia walimtolea wito mwanamke huyo kujiendeleza zaidi kitaaluma baada ya ndoa . “Wanawake, kumbukeni wakati wote kuwa huru. Usikate tamaa baada ya ndoa, jikwamue mwenyewe ,”aliandika mtumiaji mmoja wa mtandao wa kijamii. 

 

Kwa mujibu wa taasisi ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo (OECD), Wanawake wa Kichina hufanya kazi kwa saa nne kila siku bila malipo- karibu mara 2.5 zaidi ya wanaume. Ni juu ya wastani wa nchi wanachama wa OECD, ambako wanawake hutumia mara mbili ya muda wa kazi sawa na wanaume pasipoo kulipwa kwa kwa kazi yao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top