} });
 

 

Klabu ya Manchester United wamendeleza rekodi yao ya ushindi mnono kwenye Ligi Kuu baada ya kuifunga klabu ya Southampton mabao 9-0 katika Uwanja wa Old Trafford.


Wachezaji wawili wa Southampton walionyeshwa kadi nyekundu ilikuwa ni kwa Alex Jankewitz dakika ya 2 na Jan Bednarek dakika ya 86.


Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 22 kinara ni Manchester City wenye pointi 44 na wamecheza jumla ya 20.


Mabingwa watetezi Liverpool wapo nafasi ya tatu na ina pointi 40 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na Southampton ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 29.


MABAO yote 9 waliyojaza kimiani Manchester United kila mchezaji alitupia bao mojamoja mbele ya Southampton isipokuwa Martial alitupia mawili na moja la kujifunga:-

Uwanja wa Old Trafford ngoma ilikuwa namna hii:-

Aaron Wan-Bissaka dk 18

Marcus Rashford dk 25

Jan Bednareck dk 34 Og

Edinson Cavan dk 39

Anthony Martial dk 69 na 90

Scott Mc Tominay 71

Bruno Fernandes 87

Daniel James 90+3


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top