} });
 


MTANGAZAJI wa televisheni wa kampuni ya DIRECTTV, Diego Ordinhola, nchini Ecuador, alijikuta akikingiwa bastola na mtu nje ya Uwanja wa Monumental huko Tarqui, Guayaquil, ambaye alimpora simu yake na kukimbia.

 

Ordinhola ameliweka wazi tukio hilo kwenye akaunti yake ya Twitter ya Februari 12, 2021, ambalo limeonwa na watu zaidi ya 350,000  na polisi wakiapa kumtia mbaroni mhusika au walioshirikiana naye.


Katika picha iliyonaswa ya tukio hilo, mporaji anasikika wazi akisema “Simu, nipe simu yako!” ambapo baada ya kuikamata akakimbia akiwa amevaa kinyago. 

 

Ordinola na wapiga picha wenzake, walimfukuza mporaji huyo ambaye tayari alikuwa amevuka mtaa wenye patashika nyingi na alipanda bodaboda ambapo kamera zilimnasa akiwa anakimbia  na simu aliyoipora.


Mwaka jana ripota wa televisheni, Diego Demarco, alivamiwa na kuporwa simu kabla ya kuanza kurusha matangazo mubashara jijini Buenos Aires, Argentina. Hata hivyo, watu waliokuwa jirani, wakiwemo watoto, walimfukuza mtu huyo wakamkamata na kumrudishia simu mtangazaji  huyo ambaye aliwamwagia shukurani kibao.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top