} });
 


Imefahamika kuwa wawakiilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika Namungo FC itawekwa kwenye chungu cha nne, wakati wa upangaji wa makundi ya michuano hiyo mwishoni mwa juma hili mjini Cairo, Misri.

Namungo FC tayari inaongoza kwa mabao sita kwa mawili dhidi ya Clube Desportivo 1ยบ de Agosto ya Angola, huku ikisubiri mchezo wa mkondo wa pili ambao utachezwa juma hili.

Mshindi wa jumla wa mchezo huo ambaoutachezwa nchini Tanzania ataingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi, na tayari Namungo FC wametanguliza mguu moja kwenye hatua hiyo.

Michezo mingine ya hatua ya 32 ya michuano hiyo imeshakamilika na timu zimeshapangwa kwenye vyungu ambavyo vitatumika kupanga makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Chungu cha Kwanza: RS Berkane, Etoile Sahel, Raja Club Atl na  Enyimba FC

Chungu cha Pili: Pyramids FC, CS Sfaxien, ES Setif na JS Kabylie

Chungu cha Tatu: Orlando Pirates, Salitas FC, Cotonsport, Nkana FC

Chungu cha Nne: ASC Jaraaf, Al Ahli Benghazi, NAPSA Stars na Namungo SC 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top