} });
 

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu Jijini Dar es salaam ambapo Katika ziara hiyo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo.


Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Aboubakar Kunenge amesema ziara hiyo itaanza Jumatano ya February 24 ambapo Rais Dkt. Magufuli atazindua Daraja la juu Ubungo (Ubungo interchange) majira ya saa 03:30 asubuhi na Mara baada ya hapo ataelekea Mbezi kwaajili ya uzinduzi wa Kituo Cha Mabasi yaendayo Mikoani na nje ya nchi cha Mbezi Luis majira ya saa 05:30 asubuhi.

  

Aidha, RC Kunenge amesema Siku ya Alhamis ya February 25 Rais Dkt. Magufuli ataweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Soko la kisasa Kisutu majira ya saa 03:30 asubuhi na baada ya hapo atafanya shughuli ya uzinduzi wa Jengo la Jitegemee House ambapo Kuna Studio za Channel ten na Uhuru Fm.

 

RC Kunenge amesema Siku ya Ijumaa ya February 26 Mhe. Rais atafanya shughuli ya uzinduzi wa Nyumba za Polisi na Kiwanda Cha kutengeneza sare za Polisi ambapo tukio hilo litafanyika Saa 03:30 asubuhi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top