} });
 

 

Spika Job Ndugai amezitaka Kamati za Kudumu za Bunge kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kubweteka huku zikiamini muda bado upo akisema hali hiyo inaweza kusababisha zimalize miaka mitano bila kuisaidia Serikali.


Ameshauri Kamati hizo kuwatumia Mawaziri waliopo na kuhakikisha wanaanza na mambo ya msingi ambayo Wajumbe ambao ni Wawakilishi wa Wananchi wanataka yatekelezwe.

 

Aidha, ameitaka Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii kwenda kasi, hususan katika eneo la Bima ya Afya kwa wote, jambo ambalo lina manufaa kwa Watanzania.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top