} });
 


MABINGWA Watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Al Ahly, ambao wapo kundi moja na  Simba SC  wakiwa nyumbani  wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh usiku wa kuamkia leo.

 

Mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja Uwanja wa Taifa wa Cairo, mabao ya Al Ahly yalipachikwa na Mohamed Magdy dakika ya 57, Kahraba dakika ya 63 na Walter Bwalya dakika ya 71 na kuwafanya Waarabu hao sasa waongoze kundi A kwa tofauti ya mabao na Simba huku wote wakilingana pointi.

 

Mchezo unaofuata wa miamba hiyo ya Afrika ni dhidi ya Simba Februari 23, kwenye uwanja wa Mkapa Dar es salaam.soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top