} });
 


Wakili Mwandamizi Anthony Nasimire katika hotuba yake ndani ya wiki ya Sheria amesema vitendo vya hivi karibuni vya Viongozi kuwatandika viboko watu hadharani ni kinyume na Katiba na Sheria.

 

Amesema Mahakama ndio yenye ruhusa ya kutoa adhabu ikiwemo viboko ambapo Sheria imeweka marufuku viboko kutolewa hadharani `The Corporal punishment Act’ sura ya 17 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019, kifungu cha 8(5).

 

Amefafanua kuwa, kwa pamoja vitendo vya Viongozi kutandika watu viboko hadharani vinakiuka Ibara ya 13 (6) (b) ya Tanzania ya mwaka 1977 inayomhesabu mtu kuwa na haki mbele ya Sheria hadi pale kosa lake litakapothibitika Mahakamani.

 

Wito kwa walioathirika na vitendo vya baadhi ya viongozi ambao waliwapiga watu hadharani kwenda Mahakamani kwa kuwa hata adhabu ya viboko ikitolewa na mahakama huwa kuna watu maalumu wa kutekeleza adhabu hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top