} });
 


Mkazi mmoja wa Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani anashikiliwa na polisi kwa tuhuma ya kukutwa na laini 74 za kampuni mbalimbali za simu huku 56 zikidaiwa kutumika katika matukio ya utapeli na wizi. 

 

Akizungumza jana Alhamisi Machi 11, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema mtuhumiwa huyo mbali na kukutwa na laini hizo, 18 zimesajiliwa kwa jina moja la Mosses Cosmas. 

 

“Fikiria kuna Mtanzania mmoja anamiliki laini 18 amesajili kwa jina moja na ametumia kitambulisho cha Nida (cha uraia). Huu ni uhalifu mkubwa anaweza akatumia laini moja kutukana mtu, akatumia nyingine kufanya uhalifu,” amesema Nyigesa. 

 

Amesema wanawasiliana na moja ya kampuni za simu ili kujua sababu za mtuhumiwa kuwa na laini nyingi ya kampuni hiyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top