
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Godwin Mollel
amewasimamisha kazi watumishi watatu wa idara ya afya wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,
mkoani Kagera ili wapishe uchunguzi wa tuhuma ya upotevu wa dawa zilitolewa na serikali kwa
ajili ya kuwahudumia wananchi ambao utafanywa na maosa wa vyombo vya ulinzi na usalama
watakaopewa jukumu hilo.
Waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi huo ni pamoja na mganga mkuu wa halmashauri
hiyo, Bw. Revocatus Ndyekobola, Patric Yogo ambaye ni mfamasia na Gasota Bakuru, mtunza
stoo ya madawa. Mh.Mollel amesema serikali itaendelea kuwashughulikia wale wote
wanaojihusisha na wizi wa madawa yanayotolewa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma
za afya.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment