} });
 


MOJA ya headlines kali zinazotrendi kwenye gossips ni kuhusu rapa maarufu nchini Marekani, Aubrey Drake Graham ‘Drake’ kutajwa kunyemelea penzi la mwanadada mrembo kwenye tasnia ya shows na urembo, huyu si  mwingine bali ni Kim Kardashian.

 

Imeelezwa kuwa Drake ameanza kujisogeza kwa kumtumia DM Kim Kardashian kusaka fursa ya penzi tangu taarifa zianze kusambaa kuwa rapa Kanye West na mwanamama Kim wapo mahakamani kukamilisha taratibu za kupeana talaka na kuachana rasmi. 

 

Kwa mujibu wa Heat Magazine, Drake hajawahi kufahamu hasa ni kitu gani kilimvutia Kim kwa Kanye na aliwahi kuwatabiria kuwa hawatodumu katika mahusiano yao akidai kuwa Kanye sio mtu sahihi kwa Kim, lakini ameshangaa Kim kukaa muda mrefu na Kanye mpaka kupata watoto zaidi ya wawili. 

 

Drake na Kanye walishawahi kuwa na beef kali la wazi kwa miaka kadhaa huko nyuma huku Kanye akisema alitishiwa maisha na Drake. 

 

Kwa upande mwingine, inadaiwa Kanye West amem-block baby mama wake, Kim katika mawasiliano baada ya ndoa yao kufikia kilele cha kuachana. 

 

Lakini Kanye bado amekuwa akienda nyumbani kwa Kim kuwaona watoto wake pale tu Kim anapokuwa ametoka nyumbani sababu wana kundi kubwa la wafanyakazi wa ndani ambao sio wageni kwa Kanye West, hivyo wanamruhusu kuingia na kuwajulia hali watoto.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top