} });
 


NCHI za Umoja wa Ulaya na Marekani na Japan, zimesema wanasayansi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) walichelewa kufuatilia asili ya Virusi vya Corona.

 

Aidha, wamesema hawakupewa ushirikiano wa kutosha na China kwa kuwa walinyimwa uwezo wa kupata taarifa sahihi za ugonjwa huo hivyo wanaona ni vyema Uchunguzi ufanyike tena.

 

Uchunguzi uliofanywa na Maafisa wa WHO kwa wiki 4 ulitoa taarifa kwamba COVID19 haikutokea maabara bali ilisambaa kutoka kwa wanyama, hivyo China haipaswi kulaumiwa.

 

Baadhi ya nchi zilizotilia shaka ripoti hiyo ya WHO ni Marekani, Australia, Canada, Jamhuri ya Czech, Denmark, Estonia pamoja na Israel.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top