} });
 

Vipande vya ngozi vilikuwa na maandiko kutoka kitabu cha nane na cha mwisho cha kitabu cha Waebrania.

MABAKI ya machapisho ya Biblia ya kale imepatikana katika kile maafisa wametaja kuwa “uvumbuzi wa kihistoria” katika mapango ya jangwani nchini Israel. Makumi ya vipande vya karatasi ziliandikwa kwa Kigiriki, jina la Mungu likionekana kwa Kihibru.


Maneno hayo yaliandikwa kwa Kigiriki, isipokua jina la Mungu, ambalo liliandikwa kwa Kihibru.

Machapisho hayo yanayoaminiwa kuwa ya waasi wa kiyahudi waliokimbilia milimani baada ya kuibuka kwa upinzani dhidi ya utawa wa Kirumi katika karne ya pili. Zilipatikana wakati wa oparesheni ya kuhifadhi eneo hilo la pangoni lisivamiwe. 

 

Uvumbuzi huo ni wa kwanza kupatikana tangu mwanzoni mwa miaka ya 1960 wakati mabaki kama hayo na mifupa 40 ilipatikana katika eneo hilo ambale limepewa jina pango la ajabu.


Mfupa wa mtoto uliodimu, karibu miaka 6,000, pia ilipatikana

Mabaki yaliyopatikana yana machapisho kutoka ya Zakayo na Nahum, ambayo yanajumuisha sehemu ya maandiko yanayojulikana kama kitabu cha mitume 12 wadogo. 

 

Mabaki ya ngozi yalikua yameandikwa kwa Kigiriki, lugha iliyotumiwa baada ya ushindi wa Yudea na Alexander the Great katika karne ya nne kabla ya ujio wa Kirstu. Jina la Mungu, hata hivyo linaonekana kuandikwa kwa Kihibru.


Kapu kubwa linalosadikiwa kuwa la kale zaidi duniani pia lilikua miongoni mwa vitu vilivyopatikana katika pango hilo.

Mkurugenzi wa mamlaka ya mambo ya kale ya Israel (IAA), Israel Hasson amesema mabaki hayo na vitu vingine vilivyopatikana hapo ni ya “thamani kubwa ya mwanadamu”.


Sarafu iliyotumiwa na waasi wa Kiyahudi wakati wa uasi dhidi ya Roma ilipatikana.


Shehena ya shilingi za kale kutoka zama za uasi wa Kiyahudi, Mfupa wa mtoto uliodumu miaka 6,000 na kapu la kale lililotengezwa karibu miaka 10,500 iliyopita pia ilipatikana katika eneo hilo. Pango hilo lililopo chini ya mlima, haliwezi kufikiwa kirahisi isipokuwa timu ya wa wataalamu walio na ujuzi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top