} });
 


IRENE Lyimo(21) mkazi wa kata ya Kilema Kaskazini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na mwanaye wa mwaka mmoja wamekutwa wamekufa katika nyumba ya kulala wageni. 

 

Akizungumza jana Jumanne Machi 2, 2021 kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amesema mwili wa mwanamke huyo na mwanaye imekutwa juzi katika nyumba moja ya kulala wageni kata ya Marangu Magharibi.

  

Amesema mwanamke huyo aliingia kwenye nyumba hiyo akiwa na kijana mmoja, “Huyu mwanamke kuna kijana mmoja aliingia naye gesti lakini baadaye huyo kijana alitoweka hakuonekana tena mpaka huyu mwanamke alipokutwa amekufa.” 

 

Ameibainisha kuwa wanaendelea kufuatilia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kumsaka kijana huyo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top