} });
 

 

TAIFA la  Marekani jana Februari 28 imeidhinisha chanjo ya kampuni ya Jonhson & Johnson kwa matumizi ya dharura, na kuipatia nchi hiyo chanjo ya tatu ya kukabiliana na janga la virusi vya corona ambavyo vimeua wamarekani 500,000.


Mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa ya Marekani FDA, imesema kuwa chanjo ya kampuni hiyo inayotolewa kwa dozi moja ina ufanisi mkubwa katika kuzuia Covid-19 pamoja na aina mpya ya virusi cha corona.

 

Chanjo hiyo ni ya tatu kuidhinishwa kutumika nchini Marekani baada ya chanjo za Pfizer na Moderna kuidhinishwa mwezi Disemba mwaka uliopita.

 

Ithibati kutoka FDA inafuatia maoni yaliyotolewa na jopo la wataalamu huru waliosema chanjo hiyo imekidhi vigezo vya matibabu.

 

Mamlaka ya FDA imethibitisha  kuwa chanjo ya Johnson&Johnson itatolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi.

 

Kuidhinishwa kwake kunaongeza nguvu kwenye kampeni ya taifa ya utoaji chanjo nchini Marekani ambayo ilisuasua kwa wiki kadhaa.

 

Karibu watu milioni 47.2 wa Marekani tayari wamepatiwa dozi ya kwanza ya chanjo ya corona, kulingana na taasisi ya kupambana na magonjwa nchini humo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top