} });
 


Wafanyabiashara wawili wamefikishwa katika mahakama ya Wilaya Kinondoni kwa tuhuma za kukutwa na pombe ya kienyeji aina ya gongo yenye ujazo wa Lita 73.

  

Watuhumiwa hao ni Adrian Mtenga (48) na Veronica Mokili (25) wote wakiwa ni wakazi wa Tandale, ambapo wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa shtaka na wakili wa Serikali Ester Chale, Mbele ya Hakimu Mkazi, Happy Kikoga.

  

Ameelezwa kuwa Februari 3, mwaka huu eneo la Tandale washitakiwa hao walikutwa wakimiliki pombe ya kienyeji aina ya Gongo kinyume cha sheria.

  

Hata hivyo, washitakiwa walikana shtaka hilo na upande wa Jamhuri umedai upelelezi umekamilika na kuomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea maelekezo ya awali.

  

Washitakiwa wote wapo nje kwa dhamana hadi Machi 31, mwaka huu, baada ya kutimiza masharti yaliyowataka kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika, wenye barua za utambulisho na vitambulisho na waliyotakiwa kusaini hati ya Tsh. 500,000.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top