} });
 

 \

Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (ADU) linatarajia kuwafakisha Mahakamani Watu wanne akiwemo Said Mbasha na wanaodaiwa kuwa ni Wapenzi wake wawili akiwemo Mwanafunzi wa Chuo.

Watuhumiwa hao ni Mfanyabishara Joseph Dalidali (26), Mfanyabiasha Said Mbasha (24) na Mwanafunzi wa kike Allu John Murugwa (24), pamoja na Fatuma Shomari ( 24).

Mkuu wa Kitengo cha Kuzuia Dawa za Kulevya ACP Alhaj Kabaleke Salim Hassan amesema watuhumiwa hao wamekamatwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

“Mtuhumiwa Allu ambaye ni Mwanafunzi amekiri kuwa dawa za kulevya aliletewa na Mpenzi wake Mbasha, pia baada ya Mbasha kukamatwa alikutwa akiwa na Fatuma ambaye alikiri kuwa ni mpenzi wake (Allu na Fatuma wote Wapenzi wa Mbasha) baada ya kuwafanyia upekuzi katika nyumba wanayoishi walikutwa na pesa USD 14, 000 , pia wamekutwa na TSh.Mil.12.3 pamoja na misokoto 3 ya bangi”.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top