} });
 

Mbwa wa Rais wa Marekani aitwaye Meja amemng’ata mtumishi mwingine wa Ikulu, siku chache tu baada ya kurudi kutoka mafunzoni Delaware ili asirudie kitendo kama hicho alichokifanya mapema mwezi huu.

Msemaji wa Mke wa Rais wa Marekani Jill Biden, amesema kwamba kwa tahadhari kubwa mhusika wa tukio hilo la kung’atwa na mbwa alipatiwa huduma na madaktari na kisha akarudia kazi.

Mbwa Meja ni moja wa mbwa mdogo kati ya mbwa wawili wa rais Biden aina ya German Shepherds na ni mbwa wa kwanza wa Ikulu ya Marekani aliyepatikana kutokana na kuokolewa mitaani.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top