
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir amewaomba Watanzania kuondoa hofu na kumuomba Mungu wakati wote katika kipindi hiki ambacho mataifa mbalimbali duniani yanakabiliwa na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Ameeleza hayo leo Jumanne Machi 2, 2021 katika mkutano wake na
waandishi wa habari.
Amewataka wananchi kumuomba Mungu awaondolee hofu aliyodai kuwa
inadhoofisha nguvu za mwili ambayo ikipungua mtu husika anaweza kupata magonjwa
mbalimbali.
"Nawaomba watanzania katika kipindi hiki wamuombe Mungu na
waondoe hofu, wasiwe chanzo cha kusababisha hofu kwa wengine ili kuweza kukabiliana
na changamoto tunazopitia kwa sasa za magonjwa mbalimbali ikiwemo corona,"
amesema
Amewataka kufuatilia na kutekeleza taratibu zilizotolewa na Rais
John Magufuli kupitia Wizara ya Afya za namna ya kujilinda na kujikinga na
magonjwa yanayosambaa kwa njia ya hewa.
Post a Comment