} });
 

 

Rais wa Uganda’ Yoweri Museveni amesema bado anaangalia ni chanjo ipi atakayochomwa, siku chache baada serikali yake kuanza kutoa chanjo ya Oxford-AstraZeneca kwa wananchi.

 

Tayari marais wengine barani Afrika wameonesha kwa umma wakipata chanjo ili kuhakikishia usalama na ubora wa chanjo. 

 

Katika hotuba yake usiku wa kuamkia leo, Rais Museveni amesema hajapata chanjo bado kwa kuwa yuko makini na ana ulinzi wa kutosha “. Aisema mke wake, Janet Museveni,pia bado hajapata chanjo hiyo. 

 

Mwezi uliopita Waziri wa afya wa nchini humo Jane Aceng , alikanusha taarifa kuwa rais na watu wake wa karibu walikuwa wanapokea chanjo nyingine kwa siri kabla ya taifa hilo kupokea chanjo rasmi. Alitoa ufafanuzi baada ya gazeti la nchini humo la Daily Monitor na gazeti la Marekani la jarida la Wall Street. 

 

Aidha rais Museveni amelitaka gazeti hilo kuomba radhi kwa kuandika barua kwenye kurasa ya mbele ya gazeti au atawafuata. Uganda ina mpango wa kutoa chanjo kwa 49.6% ya idadi ya watu katika awamu ya kwanza. 

 

Nchi hiyo imepokea dozi 864,000 za chanjo kutoka Covax mapema mwezi huu na inatarajia kupokea nyingine 2,688,000 mwishoni mwa mwezi Juni.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top