
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Wilbroad Mutafungwa amewataka
madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda kote nchini kutii sheria za usalama barabarani
ikiwemo kupakia abiria wakiwa wamevaa koa ngumu kwa lengo la kuzuia madhara ya ajali
pindi inapotokea.
Akiongea na madereva wa bodaboda katika Halmashauri ya mji wa Makambako katika uwanja
wa jeshi la polisi mjini Makambako, kamanda Mutafungwa amesema mazoea waliyonayo
madereva hao kuendesha vyombo vya moto bila kufuata sheria za usalama barabarani
hayakubaliki.
Aidha, Kwa upande wake kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Njombe Jane
Warioba amepiga marufuku kwa madereva hao kuendesha boda boda kama huna mafunzo
wala kuwa na leseni ya udereva.
Naye mwenyekiti wa madereva boda boda Halmashauri ya mji wa Makambako kwa niaba ya
madereva hao ameliomba jeshi la polisi kuendelea kutoa elimu ya sheria za usalama
barabarani .
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment