} });
 


Timothy Dean Alsip (50) wa Oregon Marekani aliwahi kuvamia Bank na kufanya tishio la kutaka kupora USD 1 (Tsh. 2319) alifanya hivyo makusudi ili ipigwe simu Polisi na kweli Benki waliipiga huku yeye akikaa kwenye sofa kuwasubiri.

Lengo lake lilikuwa afungwe Gerezani ili akapate msaada wa matibabu, Timoth alikuwa ni ombaomba mwenye maisha magumu ambaye hakuwa hata na pa kuishi, siku ya tukio Benki alimtishia Muhudumu ampe $ 1 na akigoma atampiga risasi, Muhudumu alikimbizwa Hospitali kwa presha na Timothy akahukumiwa miezi isiyozidi 12 Gerezani.

Akiwa Mahakamani licha ya kukiri kufanya hivyo makusudi ili aende Gerezani kwa nia ya kupata matibabu ya bure ya mgongo na miguu, aliiambia Mahakama kuwa kama kifungo kitakuwa kifupi akitoka atarudia tena kosa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top